Ufunuo 9:10
Revelation 9:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao.
Revelation 9:10 in English
Revelation 9:10 · Berean Standard Bible
They had tails with stingers like scorpions, which had the power to injure people for five months.
Context
8Walikuwa na nywele kama za wanawake, na meno yao yalikuwa kama ya simba. 9Walikuwa na dirii kama za chuma, na sauti za mabawa yao zilikuwa kama ngurumo za farasi wengi na magari mengi yakikimbilia vitani. 10Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao. 11Walikuwa na mfalme wao, ambaye ni malaika wa lile Shimo, ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani ni Apolioni.* 12Ole ya kwanza imepita, bado nyingine mbili zinakuja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.