Ufunuo 9:12
Revelation 9:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ole ya kwanza imepita, bado nyingine mbili zinakuja.
Revelation 9:12 in English
Revelation 9:12 · Berean Standard Bible
The first woe has passed. Behold, two woes are still to follow.
Context
10Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao. 11Walikuwa na mfalme wao, ambaye ni malaika wa lile Shimo, ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani ni Apolioni.* 12Ole ya kwanza imepita, bado nyingine mbili zinakuja. 13Malaika wa sita akaipiga tarumbeta yake, nami nikasikia sauti ikitoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyoko mbele za Mungu. 14Ile sauti ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Frati.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.