Ufunuo 9:14
Revelation 9:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ile sauti ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Frati.”
Revelation 9:14 in English
Revelation 9:14 · Berean Standard Bible
saying to the sixth angel with the trumpet, “Release the four angels who are bound at the great river Euphrates.”
Context
12Ole ya kwanza imepita, bado nyingine mbili zinakuja. 13Malaika wa sita akaipiga tarumbeta yake, nami nikasikia sauti ikitoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyoko mbele za Mungu. 14Ile sauti ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Frati.” 15Basi wale malaika wanne, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hiyo, na siku hiyo, na mwezi huo, na mwaka huo ili wawaue theluthi ya wanadamu wakafunguliwa. 16Idadi ya majeshi wapanda farasi ilikuwa 200,000,000. Nilisikia idadi yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.