Ufunuo 9:16
Revelation 9:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Idadi ya majeshi wapanda farasi ilikuwa 200,000,000. Nilisikia idadi yao.
Revelation 9:16 in English
Revelation 9:16 · Berean Standard Bible
And the number of mounted troops was two hundred million; I heard their number.
Context
14Ile sauti ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Frati.” 15Basi wale malaika wanne, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hiyo, na siku hiyo, na mwezi huo, na mwaka huo ili wawaue theluthi ya wanadamu wakafunguliwa. 16Idadi ya majeshi wapanda farasi ilikuwa 200,000,000. Nilisikia idadi yao. 17Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: Wapanda farasi walivaa dirii vifuani zenye rangi nyekundu sana kama ya moto na yakuti samawi na kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vichwa vya simba, na moto, moshi na kiberiti vilitoka vinywani mwao. 18Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo hayo matatu, yaani, huo moto, moshi na kiberiti, vilivyotoka kwenye vinywa vya hao farasi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.