Ufunuo 7:10
Revelation 7:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema: “Wokovu una Mungu wetu, yeye aketiye kwenye kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo!”
Revelation 7:10 in English
Revelation 7:10 · Berean Standard Bible
And they cried out in a loud voice: “Salvation to our God, who sits on the throne, and to the Lamb!”
Context
8kutoka kabila la Zabuloni 12,000,
kutoka kabila la Yosefu 12,000,
na kutoka kabila la Benyamini 12,000. 9Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. 10Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema:
“Wokovu una Mungu wetu,
yeye aketiye kwenye kiti cha enzi,
na Mwana-Kondoo!” 11Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu, 12wakisema:
“Amen!
Sifa na utukufu
na hekima na shukrani na heshima
na uweza na nguvu
viwe kwa Mungu wetu milele na milele.
Amen!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.