Native Bible

Revelation 20:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hiyo miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake,

Revelation 20:7 in English

Revelation 20:7 · Berean Standard Bible

When the thousand years are complete, Satan will be released from his prison,

Context

5(Wafu waliosalia hawakufufuka mpaka ilipotimia hiyo miaka 1,000.) Huu ndio ufufuo wa kwanza. 6Waliobarikiwa na walio watakatifu ni wale walio na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Hao mauti ya pili haina nguvu juu yao, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka 1,000. 7Hiyo miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake, 8naye atatoka ili kuyadanganya mataifa yaliyopo katika pembe nne za dunia, yaani, Gogu na Magogu apate kuwakusanya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga ulioko pwani. 9Nao walitembea katika eneo lote la dunia, wakaizunguka kambi ya watakatifu na ule mji unaopendwa. Lakini moto ukashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.