Ufunuo 19:7
Revelation 19:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tufurahi, tushangilie na kumpa utukufu! Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo imewadia na bibi arusi wake amejiweka tayari.
Revelation 19:7 in English
Revelation 19:7 · Berean Standard Bible
Let us rejoice and be glad and give Him the glory. For the marriage of the Lamb has come, and His bride has made herself ready.
Context
5Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema:
“Msifuni Mungu wetu,
ninyi watumishi wake wote,
ninyi nyote mnaomcha,
wadogo kwa wakubwa!” 6Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipiga kelele wakisema:
“Haleluya!
Kwa maana Bwana Mungu wetu Mwenyezi anatawala. 7Tufurahi, tushangilie
na kumpa utukufu!
Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo imewadia
na bibi arusi wake amejiweka tayari. 8Akapewa kitani safi, nyeupe
inayongʼaa, ili avae.”
(Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.) 9Ndipo malaika akaniambia, “Andika: ‘Wamebarikiwa wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo!’ ” Naye akaongeza kusema, “Haya ndiyo maneno ya kweli ya Mungu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.