Ufunuo 19:5
Revelation 19:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema: “Msifuni Mungu wetu, ninyi watumishi wake wote, ninyi nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa!”
Revelation 19:5 in English
Revelation 19:5 · Berean Standard Bible
Then a voice came from the throne, saying: “Praise our God, all you who serve Him, and those who fear Him, small and great alike!”
Context
3Wakasema tena kwa nguvu:
“Haleluya!
Moshi wake huyo kahaba unapanda juu
milele na milele.” 4Wale wazee ishirini na wanne pamoja na wale viumbe wanne wenye uhai wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, aliyekuwa ameketi kwenye kile kiti cha enzi. Wakasema kwa sauti kuu:
“Amen, Haleluya!” 5Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema:
“Msifuni Mungu wetu,
ninyi watumishi wake wote,
ninyi nyote mnaomcha,
wadogo kwa wakubwa!” 6Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipiga kelele wakisema:
“Haleluya!
Kwa maana Bwana Mungu wetu Mwenyezi anatawala. 7Tufurahi, tushangilie
na kumpa utukufu!
Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo imewadia
na bibi arusi wake amejiweka tayari.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.