Ufunuo 11:19
Revelation 11:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.
Revelation 11:19 in English
Revelation 11:19 · Berean Standard Bible
Then the temple of God in heaven was opened, and the ark of His covenant appeared in His temple. And there were flashes of lightning, and rumblings, and peals of thunder, and an earthquake, and a great hailstorm.
Context
17wakisema:
“Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi,
uliyeko na uliyekuwako,
kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu
na ukaanza kutawala. 18Mataifa walikasirika nao
wakati wa ghadhabu yako umewadia.
Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa
na kuwapa thawabu watumishi wako manabii
na watakatifu wako pamoja na wale wote
wanaoliheshimu Jina lako,
wakubwa kwa wadogo:
na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.” 19Ndipo hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.