Native Bible

Revelation 11:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mataifa walikasirika nao wakati wa ghadhabu yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa na kuwapa thawabu watumishi wako manabii na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”

Revelation 11:18 in English

Revelation 11:18 · Berean Standard Bible

The nations were enraged,* and Your wrath has come. The time has come to judge the dead * and to reward Your servants the prophets, as well as the saints and those who fear Your name, both small and great— and to destroy those who destroy the earth.”

Context

16Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, 17wakisema: “Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu na ukaanza kutawala. 18Mataifa walikasirika nao wakati wa ghadhabu yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa na kuwapa thawabu watumishi wako manabii na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.” 19Ndipo hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.