Ufunuo 11:17
Revelation 11:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wakisema: “Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu na ukaanza kutawala.
Revelation 11:17 in English
Revelation 11:17 · Berean Standard Bible
saying: “We give thanks to You, O Lord God Almighty, the One who is and who was,* because You have taken Your great power and have begun to reign.
Context
15Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema:
“Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake,
naye atatawala milele na milele.” 16Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, 17wakisema:
“Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi,
uliyeko na uliyekuwako,
kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu
na ukaanza kutawala. 18Mataifa walikasirika nao
wakati wa ghadhabu yako umewadia.
Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa
na kuwapa thawabu watumishi wako manabii
na watakatifu wako pamoja na wale wote
wanaoliheshimu Jina lako,
wakubwa kwa wadogo:
na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.” 19Ndipo hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.