Zaburi 99:6
Psalms 99:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita Bwana, naye aliwajibu.
Psalms 99:6 in English
Psalms 99:6 · Berean Standard Bible
Moses and Aaron were among His priests; Samuel was among those who called on His name. They called to the LORD and He answered.
Context
4Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki,
wewe umethibitisha adili;
katika Yakobo umefanya
yaliyo haki na sawa. 5Mtukuzeni Bwana Mungu wetu,
na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake;
yeye ni mtakatifu. 6Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake,
Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake;
walimwita Bwana,
naye aliwajibu. 7Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu;
walizishika sheria zake na amri alizowapa. 8Ee Bwana, wetu,
ndiwe uliyewajibu,
kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,
ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.