Native Bible

Psalms 95:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote.

Psalms 95:3 in English

Psalms 95:3 · Berean Standard Bible

For the LORD is a great God, a great King above all gods.

Context

1Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu. 2Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo. 3Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote. 4Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, na vilele vya milima ni mali yake. 5Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.