Zaburi 94:19
Psalms 94:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu, faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu.
Psalms 94:19 in English
Psalms 94:19 · Berean Standard Bible
When anxiety overwhelms me, Your consolation delights my soul.
Context
17Kama Bwana asingelinisaidia upesi,
ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo. 18Niliposema, “Mguu wangu unateleza,”
Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia. 19Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu,
faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu. 20Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe,
ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake? 21Huungana kuwashambulia wenye haki,
kuwahukumu kufa wasio na hatia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.