Native Bible

Psalms 89:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa kuwa ni nani katika mbingu anayeweza kulinganishwa na Bwana? Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni aliye kama Bwana?

Psalms 89:6 in English

Psalms 89:6 · Berean Standard Bible

For who in the skies can compare with the LORD? Who among the heavenly beings * is like the LORD?

Context

4‘Nitaimarisha uzao wako milele na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ” 5Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu. 6Kwa kuwa ni nani katika mbingu anayeweza kulinganishwa na Bwana? Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni aliye kama Bwana? 7Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana, anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka. 8Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, ni nani aliye kama wewe? Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu, na uaminifu wako unakuzunguka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.