Native Bible

Psalms 80:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Matawi yake yalienea mpaka Baharini,* machipukizi yake mpaka kwenye Mto.*

Psalms 80:11 in English

Psalms 80:11 · Berean Standard Bible

It sent out its branches to the Sea,* and its shoots toward the River.*

Context

9Uliandaa shamba kwa ajili yake, mizizi ikawa imara, ukajaza nchi. 10Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, matawi yake yakafunika mierezi mikubwa. 11Matawi yake yalienea mpaka Baharini,* machipukizi yake mpaka kwenye Mto.* 12Mbona umebomoa kuta zake ili wote wapitao karibu wazichume zabibu zake? 13Nguruwe mwitu wanauharibu na wanyama wa kondeni hujilisha humo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.