Native Bible

Psalms 75:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mkononi mwa Bwana kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho.

Psalms 75:8 in English

Psalms 75:8 · Berean Standard Bible

For a cup is in the hand of the LORD, full of foaming wine mixed with spices. He pours from His cup, and all the wicked of the earth drink it down to the dregs.

Context

6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu. 7Bali Mungu ndiye ahukumuye: Humshusha huyu na kumkweza mwingine. 8Mkononi mwa Bwana kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho. 9Bali mimi, nitatangaza hili milele; nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo. 10Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote, bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.