Native Bible

Psalms 72:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto* mpaka miisho ya dunia.

Psalms 72:8 in English

Psalms 72:8 · Berean Standard Bible

May he rule from sea to sea, and from the Euphrates * to the ends of the earth.

Context

6Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanyeshayo ardhi. 7Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma. 8Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto* mpaka miisho ya dunia. 9Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi. 10Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.