Zaburi 71:19
Psalms 71:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu, wewe ambaye umefanya mambo makuu. Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe?
Psalms 71:19 in English
Psalms 71:19 · Berean Standard Bible
Your righteousness reaches to the heavens, O God, You who have done great things. Who, O God, is like You?
Context
17Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu,
hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu. 18Ee Mungu, usiniache,
hata niwapo mzee wa mvi,
mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho,
nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye. 19Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu,
wewe ambaye umefanya mambo makuu.
Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe? 20Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu,
utanihuisha tena,
kutoka vilindi vya dunia
utaniinua tena. 21Utaongeza heshima yangu
na kunifariji tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.