Native Bible

Psalms 68:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ee Mungu, ulinyesha mvua nyingi na kuiburudisha ardhi iliyokuwa imechoka.

Psalms 68:9 in English

Psalms 68:9 · Berean Standard Bible

You sent abundant rain, O God; You refreshed Your weary inheritance.

Context

7Ee Mungu, ulipowatangulia watu wako, ulipopita nyikani, 8dunia ilitikisika, mbingu zikanyesha mvua, mbele za Mungu, Yule wa Sinai, mbele za Mungu, Mungu wa Israeli. 9Ee Mungu, ulinyesha mvua nyingi na kuiburudisha ardhi iliyokuwa imechoka. 10Ee Mungu, watu wako waliishi huko, nawe kwa wingi wa utajiri wako uliwapa maskini mahitaji yao. 11Bwana alitangaza neno, waliolitangaza neno hilo walikuwa kundi kubwa:

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.