Native Bible

Psalms 68:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, yeye angurumaye kwa sauti kuu.

Psalms 68:33 in English

Psalms 68:33 · Berean Standard Bible

to Him who rides upon the highest heavens of old; behold, His mighty voice resounds.

Context

31Wajumbe watakuja kutoka Misri, Kushi* atajisalimisha kwa Mungu. 32Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia, mwimbieni Bwana sifa, 33mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, yeye angurumaye kwa sauti kuu. 34Tangazeni uwezo wa Mungu, ambaye fahari yake iko juu ya Israeli, ambaye uwezo wake uko katika anga. 35Ee Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako, Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu. Mungu Asifiwe!

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.