Native Bible

Psalms 68:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bali wenye haki na wafurahi, washangilie mbele za Mungu, wafurahi na kushangilia.

Psalms 68:3 in English

Psalms 68:3 · Berean Standard Bible

But the righteous will be glad and rejoice before God; they will celebrate with joy.

Context

1Mungu na ainuke, watesi wake watawanyike, adui zake na wakimbie mbele zake. 2Kama vile moshi upeperushwavyo na upepo, vivyo hivyo uwapeperushe mbali, kama vile nta iyeyukavyo kwenye moto, vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu. 3Bali wenye haki na wafurahi, washangilie mbele za Mungu, wafurahi na kushangilia. 4Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, mtukuzeni yeye aendeshwaye juu ya mawingu: jina lake ni Bwana, furahini mbele zake. 5Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, ni Mungu katika makao yake matakatifu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.