Zaburi 65:11
Psalms 65:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Umeuvika mwaka taji ya baraka, magari yako yanafurika kwa wingi.
Psalms 65:11 in English
Psalms 65:11 · Berean Standard Bible
You crown the year with Your bounty, and Your paths overflow with plenty.
Context
9Waitunza nchi na kuinyeshea,
waitajirisha kwa wingi.
Vijito vya Mungu vimejaa maji
ili kuwapa watu nafaka,
kwa maana wewe umeviamuru. 10Umeilowesha mifereji yake
na kusawazisha kingo zake;
umeilainisha kwa manyunyu
na kuibariki mimea yake. 11Umeuvika mwaka taji ya baraka,
magari yako yanafurika kwa wingi. 12Mbuga za majani za jangwani umezineemesha;
vilima vimevikwa furaha. 13Penye nyanda za malisho pamejaa makundi ya wanyama,
na mabonde yamepambwa kwa mavuno;
vyote vinashangilia kwa furaha na kuimba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.