Native Bible

Psalms 61:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.

Psalms 61:4 in English

Psalms 61:4 · Berean Standard Bible

Let me dwell in Your tent forever and take refuge in the shelter of Your wings. Selah

Context

2Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninaita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ule ulio juu kuliko mimi. 3Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui. 4Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako. 5Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu, umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako. 6Mwongezee mfalme siku za maisha yake, miaka yake kwa vizazi vingi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.