Zaburi 58:4
Psalms 58:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sumu yao ni kama sumu ya nyoka, kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake,
Psalms 58:4 in English
Psalms 58:4 · Berean Standard Bible
Their venom is like the venom of a snake, like a cobra that shuts its ears,
Context
2La, mioyoni mwenu mnatunga udhalimu,
na mikono yenu hupima jeuri duniani. 3Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao,
toka tumboni mwa mama zao
ni wakaidi na husema uongo. 4Sumu yao ni kama sumu ya nyoka,
kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake, 5ambaye hatasikia sauti ya kutumbuiza ya mwaguzi,
hata kama mganga angecheza kwa ustadi kiasi gani. 6Ee Mungu, yavunje meno katika vinywa vyao;
Ee Bwana, vunja meno makali ya hao simba!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.