Zaburi 56:6
Psalms 56:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wananifanyia hila, wanajificha, wanatazama hatua zangu, wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu.
Psalms 56:6 in English
Psalms 56:6 · Berean Standard Bible
They conspire, they lurk, they watch my steps while they wait to take my life.
Context
4Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu,
katika Mungu ninatumaini; sitaogopa.
Mwanadamu apatikanaye na kufa,
atanitenda nini? 5Mchana kutwa wanayageuza maneno yangu,
siku zote wanapanga shauri la kunidhuru. 6Wananifanyia hila, wanajificha,
wanatazama hatua zangu,
wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu. 7Wasiepuke kwa vyovyote,
Ee Mungu, katika hasira yako yaangushe mataifa. 8Andika maombolezo yangu,
orodhesha machozi yangu katika gombo lako:
je, haya hayapo katika kumbukumbu zako?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.