Native Bible

Psalms 55:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mwenzangu hushambulia rafiki zake, naye huvunja agano lake.

Psalms 55:20 in English

Psalms 55:20 · Berean Standard Bible

My companion attacks his friends; he violates his covenant.

Context

18Huniokoa nikawa salama katika vita vilivyopangwa dhidi yangu, ingawa watu wengi hunipinga. 19Mungu anayemiliki milele, atawasikia na kuwaadhibu, watu ambao hawabadilishi njia zao, wala hawana hofu ya Mungu. 20Mwenzangu hushambulia rafiki zake, naye huvunja agano lake. 21Mazungumzo yake ni laini kama siagi, hata hivyo vita vimo moyoni mwake. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa. 22Mtwike Bwana fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.