Zaburi 51:14
Psalms 51:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako.
Psalms 51:14 in English
Psalms 51:14 · Berean Standard Bible
Deliver me from bloodguilt, O God, the God of my salvation, and my tongue will sing of Your righteousness.
Context
12Unirudishie tena furaha ya wokovu wako,
unipe roho ya utii, ili initegemeze. 13Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako,
na wenye dhambi watakugeukia wewe. 14Ee Mungu, Mungu uniokoaye,
niokoe na hatia ya kumwaga damu,
nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako. 15Ee Bwana, fungua midomo yangu,
na kinywa changu kitatangaza sifa zako. 16Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta,
hufurahii sadaka za kuteketezwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.