Native Bible

Psalms 39:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Lakini sasa Bwana, nitafute nini? Tumaini langu ni kwako.

Psalms 39:7 in English

Psalms 39:7 · Berean Standard Bible

And now, O Lord, for what do I wait? My hope is in You.

Context

5Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi; muda wangu wa kuishi ni kama hauna thamani kwako. Maisha ya kila mwanadamu ni kama pumzi. 6Hakika kila binadamu ni kama njozi aendapo huku na huko: hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili; anakusanya mali nyingi, wala hajui ni nani atakayeifaidi. 7“Lakini sasa Bwana, nitafute nini? Tumaini langu ni kwako. 8Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote, usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu. 9Nilinyamaza kimya, sikufumbua kinywa changu, kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.