Native Bible

Psalms 39:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hakika kila binadamu ni kama njozi aendapo huku na huko: hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili; anakusanya mali nyingi, wala hajui ni nani atakayeifaidi.

Psalms 39:6 in English

Psalms 39:6 · Berean Standard Bible

Surely every man goes about like a phantom; surely he bustles in vain; he heaps up riches not knowing who will haul them away.

Context

4“Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu na hesabu ya siku zangu; nijalie kujua jinsi maisha yangu yanavyopita upesi. 5Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi; muda wangu wa kuishi ni kama hauna thamani kwako. Maisha ya kila mwanadamu ni kama pumzi. 6Hakika kila binadamu ni kama njozi aendapo huku na huko: hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili; anakusanya mali nyingi, wala hajui ni nani atakayeifaidi. 7“Lakini sasa Bwana, nitafute nini? Tumaini langu ni kwako. 8Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote, usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.