Zaburi 37:9
Psalms 37:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.
Psalms 37:9 in English
Psalms 37:9 · Berean Standard Bible
For the evildoers will be cut off, but those who hope in the LORD will inherit the land.
Context
7Tulia mbele za Bwana
na umngojee kwa uvumilivu;
usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,
wanapotekeleza mipango yao miovu. 8Epuka hasira na uache ghadhabu,
usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu. 9Kwa maana waovu watakatiliwa mbali,
bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi. 10Bado kitambo kidogo, nao waovu hawataonekana,
ingawa utawatafuta, hawataonekana. 11Bali wanyenyekevu watairithi nchi
na wafurahie amani tele.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.