Zaburi 37:6
Psalms 37:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko, na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri.
Psalms 37:6 in English
Psalms 37:6 · Berean Standard Bible
He will bring forth your righteousness like the dawn, your justice like the noonday sun.
Context
4Jifurahishe katika Bwana
naye atakupa haja za moyo wako. 5Mkabidhi Bwana njia yako,
mtumaini yeye, naye atatenda hili: 6Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko,
na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri. 7Tulia mbele za Bwana
na umngojee kwa uvumilivu;
usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,
wanapotekeleza mipango yao miovu. 8Epuka hasira na uache ghadhabu,
usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.