Zaburi 32:9
Psalms 32:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usiwe kama farasi au nyumbu wasio na akili, ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu la sivyo hawatakukaribia.
Psalms 32:9 in English
Psalms 32:9 · Berean Standard Bible
Do not be like the horse or mule, which have no understanding; they must be controlled with bit and bridle to make them come to you.
Context
7Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha,
utaniepusha na taabu
na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu. 8Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;
nitakushauri na kukuangalia. 9Usiwe kama farasi au nyumbu
wasio na akili,
ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu
la sivyo hawatakukaribia. 10Mtu mwovu ana taabu nyingi,
bali upendo usio na kikomo wa Bwana
unamzunguka mtu anayemtumaini. 11Shangilieni katika Bwana na mfurahi, enyi wenye haki!
Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.