Native Bible

Psalms 32:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha, utaniepusha na taabu na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.

Psalms 32:7 in English

Psalms 32:7 · Berean Standard Bible

You are my hiding place. You protect me from trouble; You surround me with songs of deliverance. Selah

Context

5Kisha nilikujulisha dhambi yangu wala sikuficha uovu wangu. Nilisema, “Nitaungama makosa yangu kwa Bwana.” Ndipo uliponisamehe hatia ya dhambi yangu. 6Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe wakati unapopatikana, hakika maji makuu yatakapofurika hayatamfikia yeye. 7Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha, utaniepusha na taabu na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu. 8Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; nitakushauri na kukuangalia. 9Usiwe kama farasi au nyumbu wasio na akili, ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu la sivyo hawatakukaribia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.