Zaburi 32:3
Psalms 32:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.
Psalms 32:3 in English
Psalms 32:3 · Berean Standard Bible
When I kept silent, my bones became brittle from my groaning all day long.
Context
1Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake,
ambaye dhambi zake zimefunikwa. 2Heri mtu yule ambaye Bwana
hamhesabii dhambi,
na ambaye rohoni mwake
hamna udanganyifu. 3Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa
kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa. 4Usiku na mchana
mkono wako ulinilemea,
nguvu zangu zilinyonywa
kama vile katika joto la kiangazi. 5Kisha nilikujulisha dhambi yangu
wala sikuficha uovu wangu.
Nilisema, “Nitaungama
makosa yangu kwa Bwana.”
Ndipo uliponisamehe
hatia ya dhambi yangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.