Zaburi 22:16
Psalms 22:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mbwa wamenizunguka, kundi la watu waovu limenizingira, wametoboa mikono yangu na miguu yangu.
Psalms 22:16 in English
Psalms 22:16 · Berean Standard Bible
For dogs surround me; a band of evil men encircles me; they have pierced my hands and feet.*
Context
14Nimemiminwa kama maji,
mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake.
Moyo wangu umegeuka kuwa nta,
umeyeyuka ndani yangu. 15Nguvu zangu zimekauka kama kigae,
ulimi wangu umegandamana
na kaakaa la kinywa changu,
kwa sababu umenilaza
katika mavumbi ya kifo. 16Mbwa wamenizunguka,
kundi la watu waovu limenizingira,
wametoboa mikono yangu na miguu yangu. 17Naweza kuhesabu mifupa yangu yote,
watu wananikodolea macho na kunisimanga. 18Wanagawana nguo zangu wao kwa wao,
na vazi langu wanalipigia kura.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.