Zaburi 19:10
Psalms 19:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega.
Psalms 19:10 in English
Psalms 19:10 · Berean Standard Bible
They are more precious than gold, than much pure gold; they are sweeter than honey, than honey from the comb.
Context
8Maagizo ya Bwana ni kamili,
nayo hufurahisha moyo.
Amri za Bwana huangaza,
zatia nuru machoni. 9Kumcha Bwana ni utakatifu,
nako kwadumu milele.
Amri za Bwana ni za hakika,
nazo zina haki. 10Ni za thamani kuliko dhahabu,
kuliko dhahabu iliyo safi sana,
ni tamu kuliko asali,
kuliko asali kutoka kwenye sega. 11Kwa hizo mtumishi wako anaonywa,
katika kuzishika kuna thawabu kubwa. 12Ni nani awezaye kutambua makosa yake?
Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.