Zaburi 17:9
Psalms 17:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kutokana na waovu wanaonishambulia, kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.
Psalms 17:9 in English
Psalms 17:9 · Berean Standard Bible
from the wicked who assail me, from my mortal enemies who surround me.
Context
7Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu,
wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume
wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao. 8Nilinde kama mboni ya jicho lako,
unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako 9kutokana na waovu wanaonishambulia,
kutokana na adui wauaji wanaonizunguka. 10Huifunga mioyo yao iliyo migumu,
vinywa vyao hunena kwa majivuno. 11Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira,
wakiwa macho, waniangushe chini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.