Zaburi 143:4
Psalms 143:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu, moyo wangu ndani yangu unakata tamaa.
Psalms 143:4 in English
Psalms 143:4 · Berean Standard Bible
My spirit grows faint within me; my heart is dismayed inside me.
Context
2Usimhukumu mtumishi wako,
kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako. 3Adui hunifuatilia,
hunipondaponda chini;
hunifanya niishi gizani
kama wale waliokufa zamani. 4Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu,
moyo wangu ndani yangu unakata tamaa. 5Nakumbuka siku za zamani;
natafakari juu ya kazi zako zote,
naangalia juu ya kazi
ambazo mikono yako imezifanya. 6Nanyoosha mikono yangu kwako,
nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.