Zaburi 139:14
Psalms 139:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha; kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu.
Psalms 139:14 in English
Psalms 139:14 · Berean Standard Bible
I praise You, for I am fearfully and wonderfully made. Marvelous are Your works, and I know this very well.
Context
12hata giza halitakuwa giza kwako,
usiku utangʼaa kama mchana,
kwa kuwa giza ni kama nuru kwako. 13Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;
uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu. 14Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa
kwa namna ya ajabu na ya kutisha;
kazi zako ni za ajabu,
ninajua hayo kikamilifu. 15Umbile langu halikufichika kwako,
nilipoumbwa mahali pa siri.
Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi, 16macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.
Siku zangu zote ulizonipangia
ziliandikwa katika kitabu chako
kabla haijakuwepo hata moja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.