Native Bible

Psalms 139:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utangʼaa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.

Psalms 139:12 in English

Psalms 139:12 · Berean Standard Bible

even the darkness is not dark to You, but the night shines like the day, for darkness is as light to You.

Context

10hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti. 11Kama nikisema, “Hakika giza litanificha na nuru inayonizunguka iwe usiku,” 12hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utangʼaa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako. 13Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani; uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu. 14Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha; kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.