Native Bible

Psalms 107:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.

Psalms 107:31 in English

Psalms 107:31 · Berean Standard Bible

Let them give thanks to the LORD for His loving devotion and His wonders to the sons of men.

Context

29Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono, mawimbi ya bahari yakatulia. 30Walifurahi ilipokuwa shwari, naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani. 31Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. 32Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee. 33Yeye aligeuza mito kuwa jangwa, chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.