Zaburi 106:9
Psalms 106:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka, akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani.
Psalms 106:9 in English
Psalms 106:9 · Berean Standard Bible
He rebuked the Red Sea, and it dried up; He led them through the depths as through a desert.
Context
7Wakati baba zetu walipokuwa Misri,
hawakuzingatia maajabu yako,
wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako,
bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu. 8Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake,
ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu. 9Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka,
akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani. 10Aliwaokoa mikononi mwa adui;
kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa. 11Maji yaliwafunika adui zao,
hakunusurika hata mmoja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.