Zaburi 106:21
Psalms 106:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri,
Psalms 106:21 in English
Psalms 106:21 · Berean Standard Bible
They forgot God their Savior, who did great things in Egypt,
Context
19Huko Horebu walitengeneza ndama,
na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma. 20Waliubadilisha Utukufu wao
kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani. 21Walimsahau Mungu aliyewaokoa,
aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri, 22miujiza katika nchi ya Hamu
na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu. 23Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza:
kama Mose mteule wake,
asingesimama kati yao na Mungu
kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.