Native Bible

Proverbs 5:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta;

Proverbs 5:3 in English

Proverbs 5:3 · Berean Standard Bible

Though the lips of the forbidden woman * drip honey and her speech * is smoother than oil,

Context

1Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara, 2ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa. 3Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta; 4lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili. 5Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.*

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.