Mithali 31:22
Proverbs 31:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake, yeye huvaa kitani safi na urujuani.
Proverbs 31:22 in English
Proverbs 31:22 · Berean Standard Bible
She makes coverings for her bed; her clothing is fine linen and purple.
Context
20Huwanyooshea maskini mikono yake
na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake. 21Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake,
kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto. 22Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake,
yeye huvaa kitani safi na urujuani. 23Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji,
aketipo miongoni mwa wazee wa nchi. 24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza,
naye huwauzia wafanyabiashara mishipi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.