Mithali 30:4
Proverbs 30:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? Ni nani ameshakusanya upepo kwenye vitanga vya mikono yake? Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani? Niambie kama unajua!
Proverbs 30:4 in English
Proverbs 30:4 · Berean Standard Bible
Who has ascended to heaven and come down? Who has gathered the wind in His hands? Who has bound up the waters in His cloak? Who has established all the ends of the earth? What is His name, and what is the name of His Son— surely you know!
Context
2“Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote;
sina ufahamu wa kibinadamu. 3Sijajifunza hekima,
wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu. 4Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka?
Ni nani ameshakusanya upepo
kwenye vitanga vya mikono yake?
Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake?
Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia?
Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani?
Niambie kama unajua! 5“Kila neno la Mungu ni kamilifu;
yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia. 6Usiongeze kwenye maneno yake,
ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.