Mithali 30:18
Proverbs 30:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana, naam, vinne nisivyovielewa:
Proverbs 30:18 in English
Proverbs 30:18 · Berean Standard Bible
There are three things too wonderful for me, four that I cannot understand:
Context
16Ni kaburi, tumbo lisilozaa,
nchi isiyoshiba maji kamwe,
na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’ 17“Jicho lile limdhihakilo baba,
lile linalodharau kumtii mama,
litangʼolewa na kunguru wa bondeni,
litaliwa na tai. 18“Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana,
naam, vinne nisivyovielewa: 19Ni mwendo wa tai katika anga,
mwendo wa nyoka juu ya mwamba,
mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari,
nao mwendo wa mtu pamoja na msichana. 20“Huu ndio mwendo wa mwanamke mzinzi,
hula akapangusa kinywa chake na kusema,
‘Sikufanya chochote kibaya.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.