Mithali 30:16
Proverbs 30:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni kaburi, tumbo lisilozaa, nchi isiyoshiba maji kamwe, na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’
Proverbs 30:16 in English
Proverbs 30:16 · Berean Standard Bible
Sheol, the barren womb, land never satisfied with water, and fire that never says, ‘Enough!’
Context
14wale ambao meno yao ni panga
na ambao mataya yao yamewekwa visu
kuwaangamiza maskini katika nchi,
na wahitaji kutoka miongoni mwa wanadamu. 15“Mruba anao binti wawili waliao,
‘Nipe! Nipe!’
“Kuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe,
naam, viko vinne visivyosema, ‘Yatosha!’: 16Ni kaburi, tumbo lisilozaa,
nchi isiyoshiba maji kamwe,
na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’ 17“Jicho lile limdhihakilo baba,
lile linalodharau kumtii mama,
litangʼolewa na kunguru wa bondeni,
litaliwa na tai. 18“Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana,
naam, vinne nisivyovielewa:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.