Mithali 23:8
Proverbs 23:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utatapika kile kidogo ulichokula, nawe utakuwa umepoteza bure maneno yako ya kumsifu.
Proverbs 23:8 in English
Proverbs 23:8 · Berean Standard Bible
You will vomit up what little you have eaten and waste your pleasant words.
Context
6Usile chakula cha mtu mchoyo,
usitamani vyakula vyake vitamu, 7kwa maana yeye ni aina ya mtu
ambaye kila mara anafikiri juu ya gharama.
Anakuambia, “Kula na kunywa,”
lakini moyo wake hauko pamoja nawe. 8Utatapika kile kidogo ulichokula,
nawe utakuwa umepoteza bure
maneno yako ya kumsifu. 9Usizungumze na mpumbavu,
kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako. 10Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani
wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.